BREAKING: TETEMEKO JINGINE LATOKEA KANDA YA ZIWA
BreakingNews
BREAKING: Tetemeko jingine latokea kanda ya ziwa
By Muro Tv

Ni habari za leo May 25 2017
mchana kutokea upande wa kanda ya ziwa ambako bado Wakazi wa eneo hilo
hawajasahau tetemeko lililogharimu maisha ya watu na mali zao kwa upande
wa Kagera.
Habari ya leo ni kwamba tetemeko
limeripotiwa kutokea hukohuko Kanda ya ziwa kwenye maeneo ya Mwanza na
Geita lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa mpaka sasa.
Japo halijasababisha uharibifu wowote tetemeko hilo la leo ambalo
inaripotiwa limechukua kuanzia sekunde 7-10 limesababisha baadhi ya
waliokuwemo kwenye majengo ya gorofa ambayo ni Mwanjonde Block, Administration Block, Academic Block, Library Block (Mario Mgulunde Learning Resource Centre) na Majengo mengine kutoka kwenye majengo hayo wakiwemo
Wanafunzi Pamoja na wafanyakazi wa SAUT Mwanza.
MURO TV ilikuwepo mubashara kabisa eneo la tukio, habari nzuri ni kwamba Tetemeko hilo halikuwa kubwa sana kama lile la hivi karibuni na hakuna hata mtu mmoja alieripotiwa kuumia ama kupata mshutuko uliompelekea matatizo.
MURO TV Inawapa pole watu wote wa kanda ya ziwa kwa tukio hilo
No comments:
Post a Comment