UPDATES: CCM YAZUNGUMZA MAMBO MAWILI MAKUBWA YANAYOENDELEA
SIASA
UPDATES: CCM yazungumzia mambo mawili makubwa yanayoendelea

Chama cha mapinduzi (CCM) leo May 25 2017 Dar es salaam kimezungumza na Waandishi wa habari kupitia kwa Katibu wake wa itikadi na uenezi Humphrey Polepole na kuzungumzia mambo mawili makubwa yanayoendelea.
JAMBO LA KWANZA: ‘Leo
nitazungumza mambo mawili ambayo yamekua makubwa na yanaendelea kwenye
taifa letu, moja ni swala la ulinzi na usalama wa Wananchi wetu wa
Tanzania hasa zaidi katika muendelezo wa matukio kwenye eneo la
Mkuranga, Kibiti na Rufiji‘
‘Sisi
kama chama tumelifatilia na kuona ni vyema kusimama na Watanzania
wakiwemo Wanachama wa CCM katika maeneo haya kusema tuko pamoja,
tunatambua wanapitia wakati mgumu, wapo waliopoteza maisha sio kwasababu
ya mapenzi ya Mwenyenzi Mungu… wamepoteza maisha yao kwasababu
yamekatizwa’
‘Sitaki kusema maneno makubwa kwamba
zaidi kwamba ikiendelea tutapenda kuona watu wengine wanawajibishwa..
niseme pia tumesikitishwa sana, sisi tunaamini demokrasia ya vyama vingi
ni mshikamano lakini tunahisi kama tumeachwa wenyewe, tumevunjika moyo
sana, ukimya wa wenzetu vyama vingine vya siasa umetusikitisha’
“Nimeona wenzangu wametingwa na
kufanya siasa za madaraka kuliko siasa za maendeleo na zinazohusika na
shida za watu wetu, hakuna namna nyingine nzuri ya kuwahudumia
Watanzania kama kushikamana wakati wa matatizo bila kujali tofauti zetu
za kiitikadi‘ – Polepole
JAMBO LA PILI: ‘Nalisema
hili katika namna ambayo mara nyingi watu wamezoea na ni mazoea mabaya
kwamba mtu akifanya jambo jema hatakiwi kusifiwa sababu ni wajibu wake,
leo napenda niwaambie kivingine… jambo ambalo Rais Magufuli amelifanya
jana ninawaomba kwa heshima kubwa Watanzania wote tumuunge mkono’
‘Vita zipo za aina nyingi, zipo
tunazopigana kwa silaha… mtu na mtu, nchi na nchi… wengi wamezoea hizi….
lakini zipi vita za kiuchumi, ni mbaya zaidi kuliko vita ya kupigana na
silaha, inalenga kuturudisha nyuma na kufukia malengo ya sisi kuwa
taifa huru na linalojitegemea’
‘Nawaomba Watanzania sio tu WanaCCM kwa
heshima kubwa tumuunge mkono Rais wetu mpendwa, atakua imara na
madhubuti zaidi tukisimama nae sote’
No comments:
Post a Comment