Siku moja baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la
Azam Sports Federation Cup kati ya
Simba dhidi ya
Mbao FC katika uwanja wa Jamhuri
Dodoma na
Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, leo May 28 nahodha wa timu hiyo
Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali.
Jonas Mkude
Mkude ambaye alikuwa katika gari binafsi na baadhi ya watu amepata ajali ya gari akitokea
Dodoma akiwa maeneo ya
Dumila mkoani
Morogoro akiwahi
Dar es Salaam kwa ajili ya kambi ya timu ya taifa
Taifa Stars.
Gari waliyopata nayo ajali Jonas Mkude na abiria wengine
Taarifa za awali zinaeleza kuwa
Mkude ameumia
maeneo ya shingo na amepelekwa hospitali wakati mmoja kati ya abiria
waliyokuwemo katika gari hilo akiripotiwa kupoteza maisha
MuroTv inaendelea kufuatilia taarifa hizi na itakuletea hapa.
Kutoka Kushoto ni beki wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ shabiki na Said Ndemla kiungo wa Simba SC
No comments:
Post a Comment