Mourinho afunguka kwa nini alimuacha Herrera vs Basel
Ander Herrera alicheza game yake ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu England weekend iliyomalizika Man United ikiambulia sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City lakini kiungo huyo aliachwa katika mchezo wa jana wa Champions League dhidi ya Basel.
Jose Mourinho ameweka wazi kuwa maamuzi yake hayo yalikuwa ya kiufundi wala hakuna sababu nyingine kwa sababu aliamua kutumia viungo wawili Matic, Pogba na Herrera kumuacha.
“Hakuna sababu za ziada kwa Herrera kuwa nje, game ambayo tuliamua kutumia viungo watatu Herrera alicheza lakini tulitumia viungo wawili tu Matic na Pogba na walicheza vizuri hivyo hatukuona sababu ya kufanya mabadiliko, hata hivyo Fellaini na Carrick walikuwepo benchi pia ” >>> Jose Mourinho
No comments:
Post a Comment