Waigizaji wanaolipwa Pesa Nyingi Duniani 2017
Emma Stone ndiye mwigizaji wa kike anayelipwa pesa nyingi zaidi miongoni mwa waigizaji duniani mwaka huu.
Mwigizaji
huyo aliyeigiza katika filamu iliyovuma sana mwaka huu ya La La Land
alilipwa $26m (£20m) katika kipindi cha miezi 12 kati ya Juni 2016 na
Juni 2017, sana kutokana na ufanizi wa filamu hiyo.Malipo hayo yalimfanya kuongoza katika orodha ya kila mwaka ya jarida la Forbes, na kuwashinda Jennifer Anniston na Emma Watson.
Jennifer Lawrence, aliyeongoza 2016, alikuwa wa tatu baada ya kulipwa $24m (£19m).
Mwigizaji huyo wa miaka 28 majuzi alizungumzia mjadala kuhusu pengo la mishahara kati ya waigizaji wa kiume na wa kike, ambapo alifichua kwamba waigizaji wenzake wa kiume wameamua kwa hiari kupunguziwa mishahara ndipo walipwe kiasi sawa.
Jennifer Lawrence alikuwa ameongoza orodha hiyo ya Forbes kwa miaka miwili iliyotangulia, sana kutokana na ufanisi wa filamu za Hunger Games.
Mwaka 2016 alipata $46m (£36m), baada ya kutolewa kwa The Hunger Games: Mockingjay - Sehemu ya Pili 2, makala ya mwisho ya mwendelezo wa filamu hizo.
Waigizaji wa kike hao wote walipata zaidi ya $11.5m (£9m) kila mmoja.
Jennifer Aniston alikuwa wa pili baada ya kupata $25.5m (£20m), sana kutokana na kutumiwa kwake kuuza Smartwater, mafuta ya ngozi ya Aveeno na shirika la ndege la Emirates.
Waigizaji hao wengine walikuwa ni Melissa McCarthy, Mila Kunis, Charlize Theron, Cate Blanchett, Julia Roberts na Amy Adams.
Dwayne "The Rock" Johnson aliongoza orodha ya waigizaji wa kiume Hollywood waliopata pesa nyingi $64.5m (£50m) kati ya Juni 2015 na Juni 2016.
Orodha ya mwaka huu ya waigizaji wa kiume wanaolipwa pesa nyingi zaidi itatolewa baadaye mwezi huu.
Mjadala kuhusu pengo la mishahara kijinsia katika uigizaji wa filamu umekuwa ukiendelea tangu kudukuliwa kwa mitambo ya Sony mwaka 2014.
Barua pepe zilizofichuliwa zilionesha Jennifer Lawrence na mwigizaji mwenzake Amy Adams walilipwa mishahara ya chini sana ukilinganisha na waigizaji wenzao wa kiume katika filamu ya American Hustle.
Emilia Clarke amesema ubaguzi wa kijinsia katika tasnia ya sanaa ni kama "ubaguzi wa rangi."
No comments:
Post a Comment