Mchezaji Nicolai Muller aumia akisherehekea kufunga goli
Baada ya kufunga bao pekee katika mechi dhidi ya Augsburg dakika ya nane siku ya Jumamosi, Muller aliruka ruka na kuzunguka wakati akisherehekea goli hilo la pekee.
Alianguka vibaya na alionekana kuhisi uchungu sana kabla ya wachezaji wenzake kukimbia kuungana naye.
Mkufunzi wa Hamburg Markus Gisdol amesema kilikuwa kisa cha kushangaza.
Mchezaji huyo aliumia kano za goti la kulia na klabu hiyo imesema anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa dakika saba.
"twamtakia apone haraka na tutamsaidia kadiri ya uwezo wetu."
Muller, 29, alijiunga na Hamburg kutoka Mainz mwaka 2014 na amechezea timu ya taifa ya Ujerumani mara mbili, karibuni zaidi ikiwa mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment