Utata mwingine kwa Roma.
Rapa Roma Mkatoliki amewaacha njia panda mashabiki wake kwa kile
alichokiimba katika wimbo wake mpya wa ‘Zimbabwe’ ambapo watu wengi
wameshindwa kutafsiri mashairi yalitumiwa humo huku wengine wakiangua
vilio baada ya kuona video hiyo
Katika wimbo huo Roma Mkatoliki amejaribu kuhusisha matukio
mbalimbali ya kisiasa pamoja na lile la kwake kubwa la kutekwa ambapo
hii ndiyo kazi yake ya kwanza tokea ule mkasa wake wa kutekwa kuisha na
kusababisha maumivu mengine makali kutoka kwa mashabiki zake baada ya
kuona ‘video’ yake mpya iliyojaa hisia kali za maumivu.
Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa ‘youtube’ alioweka video hiyo
mpya watu zaidi ya 668 wametoa maoni yao jinsi walivyoupokea ujio mpya
wa Roma na hizi ni baadhi tu ya zile zilizoandikwa na mashabiki wa Roma.
Pharergy Ramson: “Roma ukienda Zimbabwe harakat atazifanya nani ‘but’ ngoma iko poa hujawahi kuniangusha ila umebadirika kidogo mzee. Nadhan kwenye hii ngoma umejibu maswali ya watu wengi sana kipindi unafanya ‘show’ pale ‘Dar live’ nilitamani urudie hii nyimbo ‘but’ sikuwa na uwezo ila umefanya vizur.”
Blandina Bilau: “Simjui sana Roma wala kufuatilia nyimbo zake lakini huu wimbo umeniliza, ‘message’ imefika jipe moyo. Mtetezi wako Mungu aendelee kukutetea”
Arthur Oyaro: “Duuh ‘so sad’ na utu uzima huu machozi nimeshindwa kuyazuia,’thank’ pia kwa kunifikirisha. Viva Roma viva”
Mdachi Classic: “Nimefatilia ‘comment’ nyingi sana ila sijaona hato komenti inayozungumzia vibaya hii ngoma zaidi ni za upendo na za kuumizwa tu. ‘In short’ hii imetugusa sana pole sana kaka yupo mungu hakimu wa yote”.
Ibrahim Utenga: ”This song reflects the real prevailing situation, it’s very sensitive song, congratulations to you brother, God save you “
Ndongo Nyambalya: “Nina wasiwasi wewe Mkatoliki hicho siyo kichwa ni semi-computer, kwenye Mungu wa John na Daud hapo nimefikiria hadi najikuta nurudiarudia kusikiza, U deserve bro! Gat u! 100”.
Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki amemwagiwa sifa kedekede na mashabiki zake ambao walikuwa wamemisi kusikia na kuona kazi zake kwa kipindi kirefu tokea alipopatwa na mkasa wa kutekwa miezi michache iliyopita na kuweza kurudi katika uhalisia wake bila ya kuhofia jambo lolote litakaloweza mtokea tena mbele yake kwa ukali wa tungo zilizojaa za kufikirika.
Una nini cha kuongezea na kimfikie muhusika muandikie hapo chini kwenye comment kitamfikia moja kwa moja.

No comments:
Post a Comment