UHURU NA RUTO WAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI MKUU WA KENYA
Uhuru Kenyatta hatimaye ametangazwa mshindi wa kiti cha Urais nchini Kenya, jambo ambalo limehitimisha siku kadhaa za sintofahamu kufuatia uchaguzi mkuu uliojaa ushindani mkubwa.
Rais mteule Uhuru alitangazwa mshindi kwa kujipatia jumla ya kura 8, 203,290 au asilimia 54.27 na Mwenyekiti wa Tume y Uchaguzi Wafura Chebukati wakati mshindani wake wa karibu Raila Odinga wa NASA akimfuatia kwa kura 6, 762, 224 ambazo ni asilimia 44.74% siku ya Ijumaa Agosti 11, ikiwa ni siku tatu baada ya kura kupigwa.
"Naomba kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa Rais mteule na William Ruto Naibu Rais Mteule," alisema Chebukati huku akishangiliwa na wafuasi wa washindi hao.
Uhuru alijizolea asilimia 25 ya kura katika majimbo 35 ambapo Raila alifanya hivyo katika majimbo 29.
Chebukati alisema jumla ya Wakenya 15,073,662 walipiga kura ikiwa ni sawa na asilimia 71.91 ya waliojiandikisha.
No comments:
Post a Comment