Muda Umefika Pambano la Mayweather vs McGregor
Bado Muda kidogo Pambano lianze
Ni tambo na majigambo ambavyo vinatawala sasa baada ya kuthibitishwa kwa pambano linalosubiriwa kwa hamu baina ya Conor McGregor vs Floyd Mayweather ambao kwa mara ya kwanza tangu walipokubaliana kupambana walikutana uso kwa uso Los Angeles.
Mbele ya mashabiki wapatao 11,000 waliofurika LA’s Staples Center, Mayweather na McGregor walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu pambano lao lilipothibitishwa huku McGregor akidai atamchapa Mayweather katika round ya nne.
Kitu ambacho kilinogesha zaidi katika kukutana kwao ni kitendo cha Mayweather kuzomewa na mashabiki wake huku McGregor akimdhihaki kwa kumuita mfupi na dhaifu.
>>>”August 26, mtu huyu atakuwa hajitambui, ni mfupi mno, ni dhaifu sana…atakuwa hajitambui ndani ya round ya nne. Hana uzoefu, simhofii.” – McGregor.
Pambano la Conor McGregor vs Floyd Mayweather litapigwa 26 August, T-Mobile Arena, Las Vegas, Marekani.
ANGALIA LIVE
No comments:
Post a Comment