Header Ads

Mke wa Roma afunguka Kuhusu Mangekimambi na Roma


Kwenye mitandao ya kijamii August 30, 2017 gumzo lilikuwa post ya mke wa Roma Mkatoliki, Mama Ivan kwenye Instagram yake baada ya kuelezea kipande cha wimbo mpya wa Roma ‘Zimbabwe’ akisema kila anapokisikia hupata wivu.
Licha ya kudai kuandika maneno hayo kama utani huku wengi waliyachukulia serious hadi kupelekea Mange Kimambi kuyanasa na kisha kuyapost kwenye Istagram na kumuomba Mke wa Roma amruhusu awe mke mwenza ili amsaidie kumlinda Roma asiibiwe na wanawake wangine.
Mama Ivan aliandika Instagram>>>“Kiukweli kila nikisikiaga huu msatari napata sanaaa wivu, utani utani hivi hivi mwisho wa siku inakuwa kweli, mimi mwenyewe alinianza kiutani utani hivi hivi, yani nyie!! wanaume hawa!! Kuolewa na msanii kunahitaji moyo” 
Sasa baada ya post hiyo Mke wa Roma  kafunguka akisema hakuwa serious bali kama Roma ataamua kumuoa Mange hatakuwa na usemi kwa kuwa mwanaume ndio mwenye maamuzi ingawa amedai hategemei kuona akioa mke mwingine kwa sababu dini hairihusu.

No comments:

Powered by Blogger.