Header Ads

Breaking: Chebukati- Bado hatujatokea fomu kutoka maeneo 17

 http://cdn.kdrtv.com/wp-content/uploads/2017/04/CHEBUKATI.jpgMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Wafula Chebukati amesema tume hiyo kufikia sasa imepokea Fomu 34B, fomu za matokeo kutoka maeneo bunge kutoka maeneo 273.
Tume hiyo ilikuwa imetarajia kupokea fomu hizo kufikia saa sita leo mchana.
Matokeo kutoka kwa maeneo 17 bado yanasubiriwa, amesema akihutubia wanahabari Bomas.
Miongoni mwa maeneo ambayo matokeo hayajafika kwa tume ni Nyali, Mvita, Lagdera, Wajir Mashariki, Mandera Magharibi, Imenti Kaskazini, Kiminini, Kitui Mashariki, Ndaragwa, Mathira, Turkana Kaskazini, Kasipul, Ndhiwa, Mogirango Kaskazini na Embakasi Mashariki.
"Tutawapasha kuhusu hatua tulizopiga saa nane unusu adhuhuri.
Kwa sasa, tutarudi faraghani na kushauriana na maajenti waangalizi na maafisa wengine,” amesema.
"Nawaomba Wakenya kuwa na subira, tafadhali rejeeni kazini tukiendelea kukamilisha kazi hii.”

No comments:

Powered by Blogger.