Wimbo wa Wiz Khalifa waupiku ule Wa ''Gangnam Style'' YouTube
Na Muro Tv (Mwandishi Mr Muro)
Psy's Gangnam Style sio video inayotazamwa zaidi katika mtandao wa Youtube.
Wimbo huo maarufu kutoka Korea Kusini ulikuwa wimbo uliochezwa sana katika mtandao huo katika kipindi cha miaka mitano iliopita.Psy's Gangnam Style sio video inayotazamwa zaidi katika mtandao wa Youtube.
Kanda hiyo ya video iliopata umaarufu hadi kuweka rekodi ya wimbo uliochezwa sana katika YouTube, hatua iliofanya kampuni hiyo kuandika alama mpya ya siri ya wimbo huo.
Lakini wimbo huo sasa umepitwa na kanda nyingine ya muziki wa Wiz Khalifa na Charlie Puth see you again.
Wimbo huo sasa umetazamwa mara 2,910,770,934 hivyobasi kuipiku idadi ya watazamaji 2,898,259,059 wa Psys.
Wimbo huo uliandikiwa filamu Fast and Furious 7 ili kumuomboleza muigizaji Paul Walker aliyefariki katika ajali ya barabarani kabla ya filamu hiyo kukamilishwa.
Ikiwa na maneno ya kumuenzi Paul Walker{("it's been a long day without you my friend/ And I'll tell you all about it when I see you again"), Wimbo huo umekuwa ukipigwa sana katika mazishi nchini Uingereza.
Huku kamera zikielekezwa juu mbinguni, kuna mshororo unaosoma: ''Ni ya Paul'' na kanda hiyo inaisha.
ANGALIA VIDEO YA WIZ KHALIFA-SEE YOU AGAIN
ANGALIA VIDEO YA PSY- GANGMAN STYLE
---Endelea kukaa karibu na Mr Muro kwa mengi zaidi---
No comments:
Post a Comment