Tundu Tundu Lissu Ahofia TLS Kufutwa……Aitisha Mkutano wa Dharula wa Wanasheria
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharula
wa wanasheria nchi nzima kwa ajili ya kujadili mapendekezo na kutoa
msimamo wao dhidi ya Serikali ya kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mawakili.
Akizumza jana kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema
mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria
kwa ujumla iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao za sheria.
Alisema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na
katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria
kadri itakavyoona inafaa.
“Mabadiliko
haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa
kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu
baada ya baraza la TLS kukaa .
“Huo
ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria
kuingia kwenye siasa, jambo ambalo linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa
sababu matokeo yake ni mabaya” alisema Mh. Tundu Lissu.
Mbali na hayo Lissu aliwaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana ya kuwepo kwa chama hicho.
Mbali na hayo Lissu aliwaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana ya kuwepo kwa chama hicho.
No comments:
Post a Comment