RAY C Atangaza Kuhitaji Mpenzi Mwenye Miaka 60
Msanii Ray C amesema sasa hana
muda tena wa kuhangaika na vijana katika mapenzi na kudai anatafuta mzee
wa miaka 60 atulie naye.
Ray C amesema hayo jana kupitia kipindi cha NIRVANA wakati akihojiwa
na Deogratius Kithama na kusema sasa anatafuta mzee kuanzia miaka 60
ndiyo anaweza kuwa naye kwenye mahusiano na kusema muda wa kucheza na
vijana kwake umeshapita.
“Nimeshakuwa sana katika mahusiano na vijana naona hakuna jipya sasa
nimeamua kutoka huko na kutafuta mtu mzima angalau miaka hamsini hivi,
tena hata huyo naona bado kijana bora awe na miaka sitini hivi nitulie
naye, hawa vijana wameshanichosha mimi” alisema Ray C
Mbali na hilo Ray C alizungumzia juu ya jaribio lake la miaka ya
nyuma kutaka kubadili kifua chake na kusema ni kweli alitaka kufanya
hivyo kwani anaamini kila binadamu kuna kitu anaweza kutaka kukifanya
vile ambavyo yeye anapenda kiwe, japo jambo hilo hakuweza kulifanya.
No comments:
Post a Comment