Mbwana Samatta aanza vizuri msimu huu kwa kuifungia goli Genk ya Ubelgiji
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta leo Jumamosi ya July 29 ameingia uwanjani kuichezea timu yake ya KRC Genk katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2017/18 dhidi ya Waasland Beveren.
KRC Genk leo imecheza game yake ya kwanza katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Waasland Beveren na kulazimishwa sare ya kufungana magoli 3-3, magoli ya Genk yakifungwa na Jose Naranjo dakika ya 70, Mbwana Samatta dakika ya 80 na dakika ya 82 Shrivjers akafunga goli la mwisho.
Magoli ya Waasland yamefungwa na Olivier Myny dakika ya 45, Zinho Gano
dakika ya 47 na 90, sare hiyo sasa inakuwa ni sare ya pili mfululizo
kwa timu hizo toka zilipokutana mara ya mwisho February 7 2017 na kutoma
sare tasa, Genk na Waasland zote baada ya sare ya leo zinashika nafasi ya nne zikilingana kila kitu.
No comments:
Post a Comment