Namna ya Kuhakiki na Kuchagua Kampuni ya Biashara ya Mtandao ya Kujiunga
Na Prosper Muro
Ili kufanikiwa katika biashara ya mtandao ni muhimu sana kufahamu
namna ya kuhakiki na kuchagua kampuni sahihi ya kujiunga na kufanya nayo
kazi. Takwimu zinasema kuwa takribani 90% ya wasambazaji wa biashara ya
mtandao wanafeli. Mojawapo ya sababu kubwa ni kuchagua kampuni isiyo
sahihi zikiwemo sababu nyingine pia nyingi elimu ya biashara ikiwa kama
sababu nyingine kubwa ya watu kushindwa katika biashara hii.
Kampuni sahihi ni ipi?
Ni ile ambayo ina bidhaa bora na yenye manufaa,rahisi kuiuza na
kumshirikisha mwingine. Ni kampuni yenye uongozi bora na yenye kutoa
malipo mazuri kwa wasambazaji wake na kuwawezesha kuboresha maisha yao
kutokana na juhudi zao.
Mambo 4 ya Kuangalia Kuchagua Kampuni Sahihi ya Biashara ya Mtandao
Kuna mambo yapatayo matatu makuu ya kuangalia ili kuchagua kampuni sahihi litakalokupa nafasi kubwa ya kufanikiwa.
-
Umri wa Kampuni
Je ni muda gani kampuni imekuwa katika biashara hii. Inaaminika kuwa
kampuni zilizokaa zaidi ya miaka mitano zinadhihirisha ukomavu katika
biashara hiyo na kukupa nafasi kubwa ya ushindi na mafanikio.
Biashara yenye miaka 10 na kuendelea ni thabiti zaidi na ni komavu.
Baadhi ya makampuni yaliyopo Tanzania na umri wake ni:
- GNLD : Miaka 58 (Toka 1958)
- Forever Living Products: 38 (toka 1978)
- Trevo: Miaka 6 (Toka 2010)
- Oriflame: Miaka 49 (Toka 1967)
Ifahamike pia kampuni ikiwa maarufu sana na ni ya muda mrefu inaweza
kukupa matokeo hasi kwa kuwa hakuna wateja wapya wa kutosha kwa kuwa
wengi wanakuwa wameshaifahamu na wamejiunga tayari au wameamua
kutojiunga.
-
Bidhaa au Huduma Inayotolewa
Biashara sahihi ya mtandao yenye fursa ni lazima iwe na bidhaa au
huduma inayohitajika na yenye manufaa kwa watu kama si hivyo kampuni hii
si sahihi na ni muhimu kuiepuka.
Ukitaka kujiunga na kampuni yoyote ya mtandao hakikisha unaifahamu
bidhaa inayouza na sifa zake zote. Bidhaa yenye kutoa faida kwa watu na
yenye uhitaji. Itakuwia vigumu kumshari mtu yeyote unayempenda na
kumjali kutumia bidhaa isiyo na manufaa kwake. Kama bidhaa hiyo huwezi
kuiuza kwa mama au baba yako, basi hiyo kampuni si sahihi. Na kama ni
kinyume chake basi ikimbilie na jiunge mara moja.
-
Mpango wa Malipo
Kitu kingine cha kuangalia kwa umakini ili kufanikiwa kwa upande wa kipato ni mpango wa malipo unaotumiwa na kampuni.
Ifahamike kuwa dhumuni kuu la yeyote kujiunga na katika biashara ya
mtandao ni kupata huduma au bidhaa (matumizi) na kupata kipato cha fedha
na hata kujenga utajiri. Sehemu ya pili ya kuongeza kipato inategemea
pia mpango wa malipo unaotumika ukiachia bidhaa na uzuri wake.
Angalau mfumo ambao unakuwezesha kukuza timu kwa haraka na kufaidika na timu unayoijenga.
Makampuni mengine yanaweka kikomo cha watu wa kuwaingiza moja kwa moja katika kizazi cha kwanza au kikomo cha vizazi chini yako.
Kampuni lisilikupa kikomo cha watu wa kuwaingiza binafsi ni bora
zaidi na linakupa nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko lebye kukupa kikomo.
Kampuni lisilo na kikomo cha idadi ya vizazi chini yako au lenye kuruhusu vizazi vingi zaidi ni nzuri zaidi.
Pia viwango vya malipo vinavyotolewa kwa kuingiza wanachama wapya na
kwa manunuzi yako binafsi na manunuzi ya vizazi vyako. Kampuni lenye
kutoa viwango vikubwa litakufaa zaidi na kinakupa nafasi ya kufanikiwa
kwa haraka sana.
Angalia baadhi ya mipango ya makampuni makubwa Tanzania:
- GNLD
- FLP
- TREVO
- ORIFLAME
-
Malipo kwa Wasambazaji
Je kampuni linalipa kwa njia gani na kwa urahisi kiasi gani?
Makampuni mengine yanalupa wasambazaji benki na mengine kwa kadi za
elekronoki
Makampuni mengine yanalipa kwa mwezi na mengine yanalipa kila wiki au vyote kwa wiki na kwa mwezi.
Hakikisha kampuni unalojiunga linalipa na linalipa kwa wakayi na kwa namna iliyo rahisi kupata fedha zako.
Uluzia wale waliokwisha jiunga kama wanalipwa inavyostahili.
Uchaguzi:
Baada ya kuangalia mambo hayo manne makuu kwa kampuni husika na
kujiridhisha kuwa yamekidhi vigezo basi unaweza kujiunga na hakuna
sababu ya kuogopa. Watu wengi wenye kuangalia biashara ya mtandao
wamekuwa na hofu kubwa kujiunga. Unatakiwa kuwa na elimu juu ya biashara
yoyote duniani kabla hujaifanya na vivyo hivyo kwa biashara ya mtandao.
Kuna fursa kubwa ya mafanikio ya kipato katika biashara ya mtandao. Unatumia nguvu ya umoja katika kufanikiwa badala ya nguvu zako wewe binafsi pekee.
Bila shaka mkala hii itakuwa ya msaada katika kufanya maamuzi ya
kampuni ipi itakufaa kujiunga na inayokupa fursa ya mafanikio kifedha
pia ukiachia mbali faida unayopata kwa kutumia bidhaa au huduma.
----Prosper Muro----
No comments:
Post a Comment