Maombi ya Manji dhidi ya IGP Sirro, AG Masaju na Mkuu wa Upelelezi DSM
Mfanyabiashara maarufu na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji
na wenzake wawili wamefungua kwa hati ya dharura maombi katika Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya DSM wakiomba waachiwe kwa sababu wamekamatwa
isivyo halali.
Mbali na Yusuf Manji katika maombi hayo yaliyowasilishwa leo July 4, 2017 na kupangiwa mbele ya Jaji Lugano Mwandambo, walalamikaji wengine ni Deogratius Kisinda na Thobias Fwere ambapo wamefungua maombi hayo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, IGP Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi Kanda ya DSM.
Kwa mujibu hati ya kiapo ambayo imewasilishwa na Wakili Gudson Ndusyepo, Manji
na wenzake wanaiomba Mahakama Kuu iwaachie kutokana na kukamatwa isivyo
halali huku wakiiomba Mahakama hiyo kutoa amri ya kuwataka walalamikiwa
wawafikishe Mahakamani ili washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Katika hati hiyo, Wakili Ndusyepo amebainisha kuwa Manji na wenzake walikamatwa nyakati tofauti tofauti ambapo mlalamikaji Kisinda alikamatwa June 30, 2017 saa 10 jioni wakati Manji na Fwere walimatwa July 1, 2017 saa 5 asubuhi katika Jengo la Quality Center Barabara ya Pugu, DSM.
Manji na wenzake walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi katika ghala la Quality Motors Group ambapo kupitia hati hiyo ya kiapo, Wakili Ndusyepo amebainisha
kuwa kukamatwa kwa walalamikaji sio halali kwa sababu kosa linalodaiwa
dhidi yao linahusiana na masuala ya Kampuni ya Quality Motors ambayo inaongozwa na Wakurugenzi wake na Manji.
Mara baada ya kukamatwa kwa walalamikaji hao waliombewa dhamana lakini ilikataliwa kwa sababu zisizojulikana:>>>”Kama
Wakili wa waombaji nimefuatilia suala la dhamana hadi sasa saa 48
zimeshapita tangu walipokamatwa, lakini hawajafikishwa Mahakamani. Jambo
hilo ni kinyume na sheria.” – Wakili Ndusyebo.
No comments:
Post a Comment