Hatimae Mzee Majuto aruhusiwa kurudi Nyumbani.
kutoka muro.com na (Shaaban)
Tanga, Mchekeshaji King Majuto baada ya kulazwa hospitalini kwa
muda wa siku tatu , ameruhusiwa na kurudi nyumbani kwake baada ya
kufanyiwa upasuaji wa hernia (ngiri) mkoani Tanga.
Mke wa muigizaji huyo, Bi. Aisha Majuto amesema kwamba tatizo
lililokuwa likimsumbua mumewe lilianza siku nyingi ingawa kwa wiki
iliyopita hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi hadi kufikia kulazwa.
“Ni kweli tulikuwa tumelazwa lakini mume wangu amesharuhusiwa
na kurudi nyumbani. Tatizo ni hernia (ngiri) na ameshafanyiwa upasuaji
na anaendelea vizuri ingawa hawezi kuzungumza kwa muda mrefu”, Bi Aisha
Majuto.
Hata hivyo mama huyo amesema utachua muda kidogo mpaka muigizaji huyo arudi tena katika kazi yake ya kuigiza.
Toa. Maoni yako.. Kama ishara ya kumshukuru mwenyezi MUNGU au kuguswa na hali aliyo nayo mzee Majuto kwa sasa. Andika maoni yako hapo chini kwenye comment ..
No comments:
Post a Comment