Baada ya kejeli na utani wa hapa na pale kutoka kwa mashabiki wa
Dar es Salaam Young Africans kwa kuona wapo kimya muda mrefu wakati ambao
Simba wapinzani wao wameanza kufanya usajili, leo June 14 2017
Yanga wameingia rasmi mkataba na
‘Ninja’
Yanga leo imetangaza kuingia mkataba na beki wa timu ya
Taifa Jang’ombe ya
Zanzibar Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’
Yanga imeingia mkataba wa miaka miwili na
Ninja kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika kipindi cha miaka miwili,
Shaibu anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa
Yanga msimu huu.
Shaibu akisaini mkataba na Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri jana June 13 2017 moja kati ya mashabiki wa
Yanga Muigizaji
Ray Kigosi aliandika malalamiko yake kwa
Yanga kupitia instagram account yake kutokana na kimya cha kutofanywa usajili, ukizingatia
Simba wamefanya usajili wa wachezaji watano wakiwemo
Kapombe, Manula na
Bocco.
No comments:
Post a Comment