UTAFITI: Madhara unayoweza kuyapata kwa kuanika nguo ndani
MuroTV
Duniani
UTAFITI: Madhara unayoweza kuyapata kwa kuanika nguo ndani
Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales Australia wamegundua madhara yanayotokana na kuanika nguo ndani ambayo ni pamoja na kusababisha ugonjwa wa pumu na matatizo ya mapafu.
Wataalam hao wanadai kuanika nguo ndani kunasababisha bakteria ambao hushambulia mfumo wa upumuaji kujikusanya kwenye nguo mbichi iliyoanikwa ndani kuliko nguo iliyoanikwa nje kwa sababu bakteria hao hawakai nje kwenye jua.
Akizungumza na KidSport mmoja wa wataalamu hao Dr. Christine Cowie alisema bakteria wengi wanaosababisha ugonjwa wa pumu hupatikana ndani ya nyumba na hupendelea hali ya unyevunyevu hivyo mtu anapovaa nguo iliyoanikwa ndani hata ikiwa imekauka anaweza kupata ugonjwa wa pumu.

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;

No comments:
Post a Comment