“Tale alitakiwa kunipenda…nilikuwa msanii mkubwa kabla yake” – Chid Benz
Leo June 22, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM rapa mkongwe Bongo Chid Benzi amefunguka na kueleza kilichotokea kipindi ambacho Babu Tale alijitolea kumsaidia ili arudi kwenye hali ya zamani na kuendelea na maisha yake kama awali.
Chid Benzi amesema kuwa Babu Tale
angemvumilia na hali yake aliyokuwa nayo kabla ya kukata tamaa ingawa
anampenda na kumuheshimu kama kaka yake na hana maana kuwa alikosea
kumuacha kipindi kile.
>>>“Nilikuwa
na game yangu kitambo na Tale alitakiwa kunipenda. Angevumilia tu maana
nilikuwa msanii mkubwa kabla yake kwenye game. Kipindi nipo zangu Sober
ilikuja list ya Magezeti wapo watu wanavuta Unga, niligundua tupo wengi
kumbe sipo peke yangu.
“Tale asinitangaze kwenye
Media mimi nimerudia Madawa, yeye ni kaka yangu napenda tuishi kama
ndugu siku zote. Sikuwepo Wasafi, nilienda pale kama La Familia ila Tale
alikuwa ananisimamia kama mdogo wake tu. Nahangaika sana kupambana ili
nitoke kwenye hili janga, now am okay.” – Chid Benzi.

No comments:
Post a Comment