Header Ads

PICHA 32: SAUT-MWANZA, JOTO LA WIKI YA RESEARCH DEFENCE KWA WAHITIMU WA MWAKA 2017

MuroTV

SAUT-MWANZA

PICHA 32: WANAFUNZI WA UALIMU (BAED) MWAKA WA TATU WAKITETEA TAFITI ZAO KWA WIKI NZIMA

  14 June, 2017

Mtu wangu Kama ilivyo kawaida yetu murotv.blogspot.com na MuroTV kukuletea habari na matukio mbalimbali ikiwemo Siasa, Uchumi, Michezo, Sanaa (Muziki), Utamaduni na Habari za hivi punde (BREAKING NEWS) ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Leo MuroTv imewamulika wanazuoni katika Ndaki (Chuo kikuu) ya Mtakatifu Agustino (St. Augustine Uniniversity of Tanzania) Campas ya Mwanza na kuwakuta Wanafunzi wa Kitivo cha Elimu (Fucult of Education) wa mwaka wa mwisho wakiwa katika wiki ya kutetea Tafiti Zao (The week of Research Defence) walizofanya kuanzia June 2016-June 2017 ikiwa ni mojawapo ya sifa (Qualification) ya kila muhitimu kufanya Tafiti kulingana na masomo anayochukua.

Wanafunzi wanaonekana kuwa na mawazo na pressure ndogo ndogo japo ni zoezi la muda mfupi na wengine wamebadili hadi jina la kundi la Whatsapp (WhatsApp Group) na kuliita THE DEFENDER, Pia kuna wanafunzi wanaonekana wakiwa na furaha hasa baadhi ya waliokwisha kufanya zoezi hilo.

Whatsapp Group

 Wanafunzi wanaonekana kuwa na mawazo tofauti tofauti kuhusu zoezi hilo la kufanya tafiti (Research), kunaonekana kuwa na makundi matatu; kundi la kwanza wanasema kuwa imekuwa ni changamoto sana kwao, mmoja alinukuliwa akisema "Inakuwa ngumu kufanya vitu viwili kwa pamoja, kuhudhuria vipindi darasani ikiwemo pamoja na kufanya assignments, tests na presentation na bado muda huo huo unatakiwa ukaonane na Research Supervisor" alisema mwanafunzi huyo.

Kundi la pili wanawaonekana kufurahishwa na zoezi hilo la kufanya Tafiti, mmoja alinukuliwa akisema "Research ina changamoto ndio lakini ni fursa pia kwetu sisi kama wanafunzi wa chuo hiki kujifunza namna ya kufanya tafiti mbalimbali kwani hata tunapomaliza masomo tunakuwa na ujuzi wa kutatua matatizo mbali mbali katika jamii zetu" alisema mwanafunzi huyo.

Na kundi la tatu wanaonekana kutokuwepo kwenye upande wowote hapo juu, kwa wao zoezi la utafiti liwepo ama kuto kuwepo ni sawa tu, mmoja alinukuliwa akisema "............Research kwangu mimi naona ni kama masomo mengine ya kawaida.......hata iwepo au kutokuwepo ni sawa tu" alisema mwanafunzi huyo.

MuroTV na murotv.blogspot.com zinawatakia zoezi jema la kudefend Research na maandalizi mema ya mitihani ya wa mwisho.





 


WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGUSTINO-MWANZA MNATANGAZIWA NA SERIKALI YA WANAFUNZI KUWA JUMAMOSI YA TAR 17 JUNE, 2017 KUTAKUWA NA  GALA NIGHT,  KWA UPANDE WA WASANII ATAKUWEPO MTU MZIMA BILLNASS, DOGO JANJA NA MWANADADA NANDY.
HIVYO MNAOMBWA KUJIPANGA KUFURAHI NA WASANII TAJWA.

 SIKILIZA WIMBO MZURI UNAOPINGA ULAWITI KWA WATOTO
Song: Anza SaSa
Artist: Fresh Andy ft Stino & K-Sam

FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
 CLICK HAPA OPEN
FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM 
CLICK HAPA ➼ OPEN

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
           : prosperalphonce35@gmail.com 
Instagram: muro_tv








No comments:

Powered by Blogger.