Header Ads

PICHA 10: Mastaa Eto’o, Xavi na Puyol walivyohudhuria harusi ya staa wa zamani wa Barcelona

MuroTV

Michezo

PICHA 10: Mastaa Eto’o, Xavi na Puyol walivyohudhuria harusi ya staa wa zamani wa Barcelona

Leo Ijumaa ya June 9 2017 staa wa zamani wa timu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania golikipa Victor Valdes ameamua kuingia katika historia mpya katika maisha yake, Valdes ameamua kufunga ndoa na Yolanda Cardona.

Harusi ya Victor Valdes na mpenzi wake wa muda mrefu Yolanda Cardona ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali aliwahi kucheza nao soka kama Samuel Eto’o, Keita, Xavi, Eric Abidal, Carles Puyol na golipa namba mbili wake akicheza Barcelona Pinto.
Carls Puyol na mpenzi wake Vanessa Lorenzo
Valdes ambaye kwa sasa anaichezea Middlesbrough ya England amefunga ndoa hiyo na mpenzi wake Yolanda Cardona jijini Barcelona leo Ijumaa ya June 9 2017, kama hujui Yolanda Cardona ni model wa Colombia.

Kushoto ni Abidal na Keita
Kwa mbali mke wa Eto’o na Samuel Eto’o mwenyewe pamoja na Keita
Aliyekuwa golikipa namba 2 wa Barcelona Pinto wakati Valdes akicheza Barcelona.
Puyol na Seydou Keita

Xavi Hernandez na mkewe

No comments:

Powered by Blogger.