Jose Mourinho alitoa heshima za mwisho kwa mwili wa baba yake mzazi mzee
Jose Manuel Mourinho Felix ambaye amefariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 79 baada ya miezi kadhaa ya kuugua.
Mourinho aliungana na mkewe
Matilde, mtoto wake wa kiume
Jose Jnr na Kocha msaidizi wa
United Silvino Louro.
Jose Mourinho akisaidia kuweka bendera kwenye Jeneza lililohifadhi mwili wa baba yake
Meneja wa Manchester United akionekana mwenye huzuni wakati wa kuuaga mwili wa baba yake
Mourinho na waombolezaji wengine wakilibeba Jeneza la Felix kupeleka Kanisani
Baba yake Mourinho alifariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua kwa miezi kadhaa
Mke wa Mourinho Matilde (kulia akivalia blauzi nyeupe) akimshuhudia Boss wa United akibeba Jeneza la baba yake
Jeneza lililobeba mwili wa Mourinho Felix likiwa ndani ya gari kabla ya kupelekwa Kanisani
Kocha wa timu ya kwanza ya Manchester United Silvino Louro (katikati) alikuwepo pia kumfariji Mourinho
Kundi la waombolezaji wakiwa nje ya Kanisa mjini Setubal kutoa heshima zao kwa mlinda mlango wa zamani Mourinho Felix
Binti wa Mourinho Matilde akionekana kufadhaishwa huku akimshikilia mama yake pamoja na kaka yake Jose Jnr
Kocha wa Makipa wa United Emilio Alvarez Blanco (katikati nyuma) na Aitor Karanka (kushoto nyuma) pia walikuwepo
No comments:
Post a Comment