Header Ads

OKWI MAMBO SAFI MSIMBAZI, KUTUA JUMAMOSI KUSAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI



okwi-kaburu










  
Shauku ya mashabiki wa klabu ya Simba kumwona mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Emmanuel Okwi kutua kwenye klabu hiyo kwa mara nyingine ni dhahiri sasa imekaribia kutimia kwa hali ilivyo sasa kati ya uongozi wa Simba na Okwi.
Hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Pope kuweka wazi kuwa tayari klabu imefikia makubaliano na Okwi na jumamosi ya Juni, 24 ataingia nchini akitokea kwao Uganda kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Nimezungumza nae na tumefanya makubaliano, ataingia hapa jumamosi kusaini mkataba wa miaka miwili … Okwi ni mchezaji mzuri ambaye amekuwa akitupatia matokeo mazuri na ni mchezaji ambaye ana uwezo wa kubadilisha matokeo ndani ya sekunde moja, wote tunafahamu uwezo wake,” alisema Hans Pope.
Aidha Hans Pope amezungumza kuhusu picha aliyopiga na Okwi na kusambaa kwenye mitandao na kufanya mashabiki wa soka waamini kuwa tayari amesaini Simba na kusema kuwa alikuwa Kampala, Uganda kwa shughuli zake binafsi na ile picha walikuwa wamekutana kufanya mazungumzo

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
           : prosperalphonce35@gmail.com 
Instagram: muro_tv

No comments:

Powered by Blogger.