Header Ads

MAREKANI YAIONYA CHINA KUHUSU VISIWA BANDIA BAHARINI

MuroTv

Duniani

Marekani yaionya China kuhusu visiwa bandia baharini

  • 3 Juni 2017
Marekanai hautakubali China kuweka wanajeshi kwenye visiwa ilivyojenga Kusini mwa bahari ya China, waziri wa ulinzi wa Merekani James Mattis ameonya.
Akiongea katika mkutano wa kiusalama huko Singapore, Bwana Mattis amesema kwamba hatua ya Uchina ya kutengeneza visiwa bandia na kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika bahari ya kimataifa unahatarisha amani katika eneo hilo.
  • China yakamata chombo cha Marekani baharini
  • China yaionya Marekani kuhusu visiwa vinavyozozaniwa
Hata hivyo amesema ugomvi kati ya Marekani na Uchina unaweza kuepukika, na akaipongeza Uchina kwa juhudi zake za kukabiliana na mgogoro unaotokana na uundaji wa zana za kinyuklia nhini Korea Kaskazini.Waziri wa ulinzi wa Marekani Gen Mattis                                         Waziri wa ulinzi wa Marekani Gen Mattis
Matamshi hayo yanatolewa muda mfupi baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia majaribio kadha ya makombora mwaka huu.
  • Ndege za China zazuia ndege ya Marekani
Baraza hilo liliunga mkono kwa wingi vikwazo hivyo baada ya mazungumzo ya majuma kadha kati ya Marekani na China
 Ramani ya kusini mwa bahari ya China                                      Ramani ya kusini mwa bahari ya China 

KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
          : prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

No comments:

Powered by Blogger.