Hili lingine la Rayvanny na BASATA kuhusu mapokezi na tuzo ya BET
Siku moja baada ya mwimbaji Rayvanny kuwasili Bongo na kukutana na mapokezi makubwa Airport DSM akiwa na tuzo yake ya BET akiwa msanii kwanza wa Bongofleva kutwaa tuzo hiyo…story gumzo ni kuhusu kutooneakana mwakilishi wa BASATA Airport.
255 ya XXL ya Clouds FM leo June 29, 2017 imempata Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza ambaye
ameelezea sababu za kutoonekana mwakilishi wa Baraza hilo akisema
kulikuwa na mawasiliano finyu kati ya Rayvanny na BASATA wakati
anakwenda na kurudi kuchukua tuzo hiyo.
>>>“Hakukuwa
na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini
tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna
budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima.
“Kwa hiyo, hakuna sababu ya
kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu
anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka
ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi
tuwapokee.” – Godfrey Mngereza.
Wakati huo huo Rayvanny amefunguka
akidai kuwa sasa hivi kila kitu kipo wazi kutokana na mitandao lakini
pia BASATA walitakiwa kusoma chochote kipindi tu walipoona amechaguliwa
kwa kuwa ndio wazazi wa muziki wa Bongofleva na kama viongozi wao
walipaswa kutoa support.
>>>“Kwa
mafano, mimi nilivyochaguliwa kama BASATA walikuwa wameona. Wao ni
wazazi walikuwa na chochote cha kusema lakini wakisema kwamba wanasubiri
niende mimi mwenyewe au tunasubiri watuambie au hatuwezi kwenda kwa
sababu hatujaambiwa. Wale ni wakubwa kwetu ni wazazi wetu tunategemea
kwamba wanakuza sanaa yetu na sisi tunawaangalia wao walitakiwa kuwa
kipaumbele sisi kutusaidia.” – Rayvanny.
No comments:
Post a Comment