#BREAKING: Waziri wa mambo ya ndani azuia wa Makinikia kwenda nje ya nchi
Leo
June 12, Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya pili ya mchanga wa madini
ambayo imebaini uwepo wa mikataba mibovu inayoitia hasara serikali
ambapo kamati imetoa mapendekezo 21 ikiwemo kuchukuliwa hatua kwa wote
waliohusika na ubadhirifu huo.
Ripoti
iliyonifikia muda huu kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu
Nchemba amewazuia wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutoka nje ya
mipaka ya Tanzania hadi vyombo vya dola vitakapofanya kazi yake kwa
mujibu wa agizo la Rais JPM.
Waziri Mwigulu amesema>>>
“Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi
wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao. Hongera sana Mh. Rais kwa
uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu
>>>Naelekeza
wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu
isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo
ya Rais kwa utimamu<<< Waziri Mwigulu Nchemba MuroTV na murotv.blogspot.comzipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati. KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;
No comments:
Post a Comment