Header Ads

BREAKING: JPM AMTEUA MPINZANI KUWA MKUU WA MKOA KILIMANJARO

MuroTv

Mix

BREAKING: JPM kamteua mpinzani kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro

 
Rais Magufuli leo June 3, 2017 amemteua Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadiki aliyejiuzulu.
Wakati huo huo, JPM amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kadhalika, JPM amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.

No comments:

Powered by Blogger.