#BREAKING: Hautawaona Halima Mdee na Ester Bulaya Bungeni hadi 2018
Leo
Jumatatu June 5, 2017 Ripoti kutoka Bungeni Dodoma zimeeleza kuwa Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imewapa adhabu ya kutohudhuria
vikao vyote vya Bunge linaloendelea hadi Bunge la Bajeti 2018/2019
Halima Mdee na Ester Bulaya.
Wabunge
hao walituhumiwa na Bunge kudharau Kiti cha Spika na kuzuia Askari
waBunge kufanya kazi zao ikiwemo kufata maagizo ya Spika Ndugai kumtoa
nje John Mnyika aliyekuwa akibishana naye kwa kutaka muongozo.
Kwa
kuzingatia maazimio hayo ya Bunge, Wabunge hawa watarejea kwenye vikao
vya Bunge katika vikao vya Bunge la Bajeti mwaka 2018 Halima Mdee na
Esther Bulaya wamepewa adhabu hii baada ya kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge kuwakuta na hatia ya kudharau Mamlaka ya Spika.
Mbunge wa
Kawe, Halima Mdee amebainika kuvunja kanuni ya 60 (1) (2) ikisomwa
pamoja na kanuni ya 74 (1) (a) na (b) na kifungu cha 26 (d) cha Sheria
ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296 kwa kufanya vitendo vya
kudharau mamlaka ya Spika.
Wakati
Esther Bulaya amebainika kuvunja kanuni ya 60 (1) (2) kanuni ya 66 (3)
(a) (b) na (c) zikisomwa pamoja na Kanuni ya 74 (1) (a) na (b) na
kifungu kifungu cha 26 (d) cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za
Bunge, Sura ya 296 kwa kufanya vitendo vya kudharau mamlaka ya Spika.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
: prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
: prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

No comments:
Post a Comment