WATANZANIA WAWILI WATAJWA JARIDA LA FORBES, UNDER 30 AFRICA
Burudani
Watanzania wawili watajwa Jarida la Forbes, Under 30 Africa
By

Kila mwaka Jarida maarufu la Forbes
ambalo hufuatilia maisha ya watu maarufu duniani na kutoa takwimu
mbalimbali zikiwepo watu wanaoingiza pesa nyingi zaidi duniani, mastaa
wanaoongoza kwa malipo ama wajasiriamali wa kutazamiwa.
Mwezi huu
Forbes Africa limetoa list ya Wajasiriamali waafrika 30 wenye umri chini
ya miaka 30 ambao wamefanya mabadiliko makubwa kwenye sekta zao na
wanafanya vizuri kama wafanyabiashara wenye umri mdogo. Mrembo Jokate Mwegelo, Lavie Makeup na Godfrey Mwagilla wametajwa kwenye jarida hilo kama wajasiriamali wakutazamwa.
No comments:
Post a Comment