TAARIFA KUTOKA IKULU DAR ES SALAAM
Mix
Taarifa kutoka IKULU Dar es salaam asubuhi hii
Taarifa hiyo iliyosambazwa saa kumi na mbili kasoro ni kuhusu uteuzi uliofanywa leo May 24 2017 na Rais Magufuli ambapo Tixon Tuliangine Nzunda ameteuliwa kuwa Naibu katibu mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) anaeshughulikia Elimu.
Kabla ya uteuzi huo Tixon alikua Katibu tawala wa mkoa wa Rukwa ambapo anakuja kuchukua nafasi ya Benard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa na uteuzi huu unaanza mara moja.

No comments:
Post a Comment