HABARI MAGAZETINI: ATUPELE KUSAINI MIAKA 2 SINGIDA UNITED
MuroTv
ATUPELE KUSAINI MIAKA 2 SINGIDA UNITED
Mchezaji huyo ambaye kwenye msimu uliomalizika hivi karibuni alikuwa kwenye kikosi cha JKT Ruvu, tayari yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Singida kwa ajili ya kusaini mkataba huo.
Akizungumza na BINGWA jana, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Singida United, alisema mchezaji huyo ni miongoni mwa matakwa ya kocha wao Hans van der Pluijm ambaye anavutiwa sana na mchezaji huyo.
Alisema usajili wa mchezaji huyo utakuwa ni wa pili kwa wachezaji wa ndani baada ya wiki iliyopita kuingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji wa zamani wa Mbeya City, Kenny Ally.
“Atupele atasaini mkataba wa miaka miwili muda si mrefu, kwani tayari tumeshafanya naye mazungumzo kilichobaki ni kuingia mkataba huo na mchezaji huyo atakuwa wa pili kwa wachezaji wa ndani baada ya hivi karibuni kumsainisha Kenny Ally,” alisema mtoa habari huyo.
Atupele ni mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye pia ameshawahi kuichezea Coastal Union ya Tanga na Ndanda FC ya Mtwara.
No comments:
Post a Comment