HABARI MAGAZETINI: WAKENYA WASAKA SAINI YA KIPA WA MBAO
MuroTv
WAKENYA WASAKA SAINI YA KIPA WA MBAO
Sony Sugar imeonyesha nia ya kumsajili kipa huyo na tayari mazungumzo ya awali yamefanyika lakini kuna klabu nyingine za Ligi Kuu Bara zimeanza kumnyemelea.
Haule alisajiliwa na Mbao katika dirisha dogo msimu huu, akitokea Panone FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ndiye aliyedakia timu yake katika mechi zote za FA walipokutana na Yanga na Simba ikiwamo ya fainali juzi.
Akizungumza na BINGWA, kipa huyo alisema baada ya kumalizikia kwa ligi huenda asiendelee kuichezea klabu kwa kuwa anahitajiwa na timu ya Sony Sugar na nyingine za Tanzania.
Alisema tayari wameshafanya mazungumzo ya awali na klabu hiyo na walikuwa wanasubiri Ligi Kuu Bara ifikie ukongoni ili wamalizane.
“Licha ya kuwa kuna timu nyingine za hapa nyumbani zinanihitaji na viongozi wake wameanza kunipigia simu, naipa kipaumbele Sony Sugar kwa sababu malengo yangu ni kucheza nje ya nchi ila nitaangalia na makubaliano na dau lao litakavyokuwa,” alisema.
Alisema wakati wa mapumziko ya mzunguko wa kwanza ikiwa ndio amesajiliwa na Mbao, walienda kucheza mechi ya kirafiki na klabu hiyo ndipo wakavutiwa naye kumwambia baada ya ligi wanamhitaji.
Ligi ya Kenya kwa sasa inaendelea na huenda kipa huyo akamwaga wino katika usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment