AJALI: Moto wateketeza bweni na kuua wanafunzi 7 Kenya
Wanafunzi saba katika Shule ya Wasichana ya Moi ‘Moi Girls High School’ iliyopo Nairobi, Kenya wameripotiwa kufariki baada ya moto kuteketeza bweni huku wengine 10 wakijeruhiwa na kulazwa Hospitalini kwa matibabu.
Kwa mujibu wa maafisa wa Msalaba Mwekundu kati ya majeruhi 10, wawili wako mahututi NA wenzao nane hawako katika hali mbaya sana na hadi sasa wanafunzi 10 wamerodheshwa kuwa hawajulikani waliko.Waziri wa Elimu wa Kenya Fred Matiang’i ameamuru shule hiyo ifungwe kwa muda wa wiki mbili huku kundi la wataalam wakifika shuleni hapo kubaini chanzo cha moto huo.
No comments:
Post a Comment