Mshtuko na hofu wakumba kijiji kimoja Afrika Kusini katika kisa cha ulaji nyama ya Binadamu
Hofu imekumba
kijiji cha Shayamoya katika jimbo la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini,
baada ya kupatikana kwa maiti ya binadamu iliyonyofolewa myama yote.
Familia
ya Zanele Hlatshwayo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ametoweka tangu
mwezi Julai mwaka huu, ikiaminika kuwa ni mhasiriwa wa genge la watu
walaji nyama ya binadamu, ambapo tayari watu watano wamekamatwa.Mwili wa mwanamke huyo ambo ulikuwa umeoza, ulipatikana baada ya mwanamume mmoja kudai kuwa mganga wa kienyeji, kuamua kujisalimisha kwa polisi juma lililopita, na kukiri kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Polisi nchini Afrika kusiri awali walipuuza taarifa hiyo.
Waliamua kukubali taarifa hiyo baada ya mtu huyo kutoa mkono na mguu wa binadamu uliojaa damu kama ushahidi, hapo ndipo alipokamatwa mara moja na maafisa wa polisi.
Aliwaongoza hadi katika nyumba ya kukodishwa, ambapo polisi walipata masikio 8 ya binadamu, ndani ya chungu cha kupikia.
Inaaminika kuwa zingetumika kuwalisha wateja wakeambao wanaaambiwa yana nguvu za miujiza ya kumpa mtu pesa, nguvu na ulinzi wa kutosha.
Viungo vingine kadhaa vya mwili wa binadamu vilipatikana ndani ya mkoba.
Majabali
Maiti ya Bi Hlatshwayo uliojaa damu na mavazi yaliyokuwa yameraruka, ulipatikana miongoni mwa viungo vingine vya binadamu nyumbani mwa mganga huyo wa kienyeji.Mavazi ya mwanadada huyo yalitambuliwa mara moja na jamaa zake.
Hata hivyo, polisi wangali wakisubiri matokeo ya uchunguzi wa DNA, ili kuthibitisha ikiwa mabaki ya maiti ni ya mwanamke huyo wa mvulana wa miaka miwili.
Familia ya Bi Hlatshwayo, bado haijamzika.
Mara nilipoingia kwwenye maskani ya Hlatshwayo, nilisalikumbana na nyimbo za huzuni na vilio kutoka kwa jamaa zake waliokuwa wakiomboleza
"Tunajaribu
kuwaza tu namna alivyokuwa akiomba kutoumizwa au kuuwawa muda mfupi
kabla ya kifo chake, alikufa kifo kibaya," alissema dadake mkubwa
Nozipho Ntelele, huku akifuta machozi.
"Mavazi yake yalikuwa yamefunikwa kwa nyasi na
vumbi, ambayo ni ishara tosha kuwa alipambana na wauwaji wake katika
harakati za kunusuru maisha yake," aliongeza Bi Ntelele.Harufu mbaya
Mganga huyo wa kienyeji anaishi katika nyumba moja ya kukodisha huko Rensburgdrift karibu na mji wa Estcourt.Jina lake la utani ni "Mkhonyovu" inayomaanisha "Mtu mfisadi au tu mfisadi" katika lugha ya Ki-Zulu.
Amekodisha nyumba hiyo kutoka kwa Philani Magubane, ambaye kakake pia amekamatwa na maafisa wa polisi, kwa kuwa mshirika wa karibu wa mganga huyo wa kienyeji.
No comments:
Post a Comment