Everton yaiganda Man City nyumbani
![]() |
Wayne Rooney amefikisha jumla ya magoli 200 katika ligi kuu ya nchini England |
Matajiri wa jiji la Manchester klabu ya Man city,imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Everton.
Everton almaarufu kama The Toffes, ndio walianza kuzifumania nyavu za Man City, kwa goli lilifungwa na mshambuliaji Wayne Rooney, Rooney amefikisha idadi ya magoli 200 katika michezo ya ligi kuu nchini England.
Katika dakika ya 82 Man City, walisawazisha goli hilo kupitia kwa winga Raheem Sterling aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Everton, Jordan Pickford.
![]() |
Raheem Sterling akipiga shuti lililokwenda moja kwa moja nyavuni |
No comments:
Post a Comment