BREAKING: Paul Kagame ashinda asilimia 98.78 ya kura
Rais wa Rwanda Paul
Kagame amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa wiki iliopita na tume
ya uchaguzi nchini humo kulingana na chombo cha habari cha AFP.
AFP
imeripoti kwamba tume hiyo ilimuongezea rais Kagame asilimia ya kura
alizopata kutoka 98.63, ikiwa ni takwimu zilizotangazwa hapo awali hadi
asilimia 98.79.Alikabiliana na wapinzani wawili , ambapo hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa kupata asilimia moja ya kura
Rais huyo amekuwa madarakani tangu 2000 na amekosolewa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.
No comments:
Post a Comment