Header Ads

Itazame safu ya bodi na menejimenti ya ACACIA Mining Tanzania kisha utaelewa tatizo liko wapi

 
Hoja yangu inajikita zaidi kwenye eneo la LOCAL CONTENT & PARTICIPATION BILL na ACT ambayo inatayarishwa

Manzoni hili jambo lilikuwa linahusu makampuni ya OIL AND GAS pekee lakini mheshimiwa Rais alisema anataka haya mambo ya uweszeshaji wa Tanzania liwe kwenye kila sekta kwenye hii nchi.

Sasa haya makampuni kama ACACIA wanaweza kuleta uhuni wa kujaza watanzania kwenye kufanya kazi za kusafisha vyoo na kazi za hali ya chini ili ku meet hiyo quota ya kuajiri wa Tanzania lakini kwenye bodi na management wako wao na token locals kama inayoonyesha hapo chini.

Haikatazwi haya makampuni kuja lakini lazima sheria iseme wazi kuwa unaweza kuja na management yako lakini no 2 lazima awe mTanzania ili baada ya miezi 6 hao wagon waondoke.

Bodi yao ina mtanzania mmoja tuu anaitwa balozi Juma Mwapachu

Tazama hapa chini:

Board of Directors

[​IMG]
JUMA MWAPACHU

Huyu naona ndio kiungo chao Tanzania na mambo ya Government relations etc. Sijajua ana shares ngapi hapo Accacia (hakuna dhambi kwa Mtz kuwa shareholder) lakini inawezekana vipi hii kampuni iwe isha operate Tanzania kwa zaidi ya miaka 2 owe imejaa wazungu na foreigners kwenye hiyo bodi?

Sasa ukija kwenye menejimenti yao utashangaa zaidi kuona kuwa mtanzania ni mmoja tuu (Deodatus Mwanyika) na kazi yake ni hiyo propaganda aka PR. Hivi mnataka kutuambia kuwa hakuna watanzania waliosoma na wenye uwezo wa kufanya hizi kazi wanazofanya hawa wazungu?

[​IMG]

DEODATUS MWANYIKA


Menejimenti hii hapa:

Management Team

Huko kwenye migodi yao sijajua nafasi wanazo nani lakini wana JF mkae mkijua kuwa hili tatizo sio ACACIA MINING pekeee bali ni makampuni mengi makubwa ya nje yanayo operate Tanzania.

Sasa ngoja ninny kwenye makampuni ya oil and gas ili mpate kuona tulips kama nchi. Yaaani kazi za kufanywa na wa Tanzania tena ambao ni wana experience, capable, competent na wana elimu zinafanywa na wageni na vibali vinatoka.

Kuna umuhim sana tukawa na sheria ya uweszeshaji wazawa au local content ama sivyo hali itazidi kuwa mbaya zaidi ya tuliyonayo kwa sasa.

Nikuulizeni mfano tuu wa huyu Peter Galeta ambaye cheo chake ni HEAD OF PEOPLE hapo ACACIA...hivi manta kutuambia kuwa hakuna mtanzania mwenye elimu, uzoefu,uwezo wa kuwa HEAD OF PEOPLE?

Tazama profile yake
[​IMG]



Peter Geleta

Hii inawezekana sana ni kuthubutu tuu. Utashangaaa haya makampuni mpaka ma secretary nao tunaletewa kutoka India, Filipino na kwingineko na wanapewa permits za kufanya kazi ambazo wapo watanzania wengi wenye uwezo wa kuzifanya

Haiwezekani mkalalamika wachina, wakenya na wahini kujazana kila mahala huku mnanyamaza wakiajiriwa kuchukua kazi za watanzania kwenye haya makampuni
 

No comments:

Powered by Blogger.