Dubai imezindua Magari yasiyotumia dereva yanayoweza kufuatilia wahalifu
Polisi wa Dubai wameanzisha program maalum kutumia magari
yasiyokuwa na dereva na yenye kamera maalum kufanya doria kwenye miji
mikubwa na sehemu zenye mikusanyiko ili kukabiliana na matukio ya
kihalifu kwa haraka.
Program hiyo itatumia magari hayo yenye uwezo wa kukimbia kwa kasi ya
9.3 mph, kutambua sura za wahalifu wanaotafutwa, kamera aina ya drone
inayoweza kumfuatilia mhalifu alipokimbilia na kutambua namba za magari
yaliyoibiwa.
Magari hayo yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayoweza kunasa
matukio yasiyokuwa ya kawaida kutoka umbali wa futi 330 na kutuma
taarifa kupitia simu za mkononi kwa Maafisa wa Polisi walio kwenye vituo
vya Polisi vilivyo karibu.
No comments:
Post a Comment