Header Ads

Penati zawaondoa Ureno Kombe la Mabara vs Chile (PICHA + VIDEO)


Mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Kombe la Mabara inayoendelea nchini Urusi ilichezwa kati ya Ureno ambao ni Mabingwa wa Euro 2016 na Mabingwa wa bara la America timu ya taifa ya Chile katika uwanja wa Estadio Olimpico Fisht.



Mchezo huo ambao ni nusu fainali ya kwanza ulichezwa kwa dakika 90 na kumalizika kwa sare tasa ndipo muamuzi akaongeza dakika 30 za nyongeza bila kupata mshindi na mikwaju ya penati ndio ikampa Chile nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya Kombe la Mabara.

Chile wanafuzu kucheza fainali ya Kombe la Mabara kwa ushindi wa mikwaju ya penati 3-0, golikipa wa timu ya taifa ya Chile Claudio Bravo ndio alikuwa shujaa wa Chile kwa kufanikiwa kucheza penati zote tatu za Ureno ambazo zilipigwa na Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Luis Nani.

Mikwaju ya penati iliyopigwa na Arturo Vidal, Charles Aranguiz na Alex Sanchez kwa upande wa Chile ndio iliwawezea kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Mabara, nusu fainali ya pili kati ya Ujerumani dhidi ya Mexico itachezwa June 30 katika uwanja wa Estadio Olimpico Fisht na mshindi wa game hiyo atacheza dhidi ya Chile fainali.
ANGALIA PENALTIES HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.