Mfanyakazi aliyefutwa awaua waliokuwa wafanyakazi wenzake 5 Marekani
MuroTV
MAREKANI
Mfanyakazi aliyefutwa awaua waliokuwa wafanyakazi wenzake 5 Marekani
John Rubet Neumann 45 alikuwa amejihami kwa bunduki na kisu
Mfanyakazi mmoja
alirudi katika kiwanda alichokuwa akikifanyia kazi bbada ya kufutwa na
na kuwaua kwa kuwapiga risasi kichwani waliokuwa wafanyakazi wenzake
kabla ya kujiua.
John Rubet Neumann 45 alikuwa amejihami kwa
bunduki na kisu wakati aliingia katika biashara moja karibu na Orlando
huko Florida siku ya Jumatatu asubuniMwanajeshi huyo wa zamani wa Marekani alifutwa kazi mwezi Aprili, kwa mujibu wa polisi.
Wengi wa wale waliouwawa walipigwa risasi kichwani.
Alikuwa akiwachagua wale aliowapiga risasi, polisi walisema.
Waliouwawa ni pamoja na Robert Snyder, 69, Brenda Montanez-Crespo, 44, Kevin Clark, 53, Jeffrey Roberts, 57, na mtu mwingine ambaye hakutambuliwa
.Mamlaka zinasema kuwa hakuwa na leseni ya kumiliki bunduki.
Aliondoka katika jeshi la Marekani mwaka 1999.

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati

No comments:
Post a Comment