Hatimae Ben Pol akutana na Ebitoke, ‘Wengi wameoa, kuolewa na wasiowapenda’
Sasa leo June 23, 2017 kupitia Instagram yake Ben Pol ameweka picha akiwa na Ebitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake.
“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika?
“Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo.
KAMA HUKUANGALIA VIDEO YA EBITOKE AKIMLILIA BEN POL CLICK HAPA CHINI KUITAZAMA
No comments:
Post a Comment