HABARI MAGAZETINI: SIMBA TUMERUDI TENA
MuroTv
SIKU moja baada ya Simba kupata tiketi ya kushiriki michuano ya
kimataifa mwakani, Wekundu hao wa Msimbazi wameanza jeuri kwa kusema
wamerudi kuwafuta jasho Watanzania.Simba ilikata tiketi hiyo juzi baada ya kuwafunga Mbao kwenye mchezo wa
fainali uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma.
Akizungumza na BINGWA, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, alisema ubingwa huo umetoa kiu ya kila shabiki Simba. Tshabalala alikwenda mbali zaidi kwa kusema ubingwa huo ni wa historia na wanaimani watapeperusha vema bendera ya taifa.
“Tumerudi kimataifa, naamini ni kiu ya muda mrefu ya kila shabiki wa Simba, huu ni ubingwa wa kihistoria,” alisema.
Wakati Tshabalala akiyasema hayo, straika Fredrick Blagnon, alisema haikuwa rahisi kupata ushindi huo na bao lake amelitoa kama zawadi kwa mashabiki wa timu hiyo.
“Najisikia vizuri sana kuweza kuifungia timu yangu, naamini haikuwa kazi rahisi kupata ushindi huu,” alisema Blagnon.
Simba kwa mwaka wa tano sasa imeshindwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuzidiwa akili na wapinzani wao Yanga na Azam, ambao walikuwa wakipokezana kwa zamu. Kitendo cha kuibuka ushindi kwenye mchezo huo na Mbao Simba sasa itaweza kupanda ndege mwakani ikiwa sambamba na Yanga ambao nao kupata tiketi baada ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu.
SIMBA: TUMERUDI TENA

No comments:
Post a Comment