Header Ads

HABARI MAGAZETINI: MUUAJII SIMBA AWAITA YANGA MEZANI

 MuroTv

MUUAJI WA SIMBA AWAITA YANGA MEZANI

MSHAMBULIAJI wa kati wa timu ya  Tanzania  Prisons aliyewatoa jasho Simba, Victor Hangaya, amewaambia mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, kama wanahitaji saini yake wakae chini wamalizane naye.

 Hangaya ameyasema hayo mara baada ya kuwapo taarifa za ndani kutoka Yanga  kumhitaji kwa ajili ya kuboresha kikosi chao kitakachoiwakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika. Akizungumza na BINGWA jana, Hangaya alisema yupo tayari kufanya kazi na Yanga kama kweli watakuwa wanamhitaji wakae mezani na kama watakuwa tayari kukubaliana naye pamoja na kumalizana na klabu yake ya Prisons.
“Nimekuwa nikisikia taarifa pamoja na kupigiwa simu kuulizwa kuhusu suala hili la kutakiwa na Yanga, bado sijaanza nao mazungumzo ila kama watakuwa tayari kufanya kazi na mimi, waje tukae mezani tuyamalize,” alisema.
Alisema malengo yake msimu ujao ni kufanya makubwa zaidi ya msimu huu ikiwamo kubeba kiatu cha ufungaji bora msimu ujao pamoja na kuendeleza rekodi ya kuwafunga vigogo.
Hangaya ambaye msimu uliopita wa 2016-17 anakumbukwa kwa kuwafunga mabao mawili Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ulioisha kwa Prisons kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

No comments:

Powered by Blogger.