Header Ads

ALICHOJIBU MADEE KUHUSU COMMENT YA ZARI KWENYE PICHA YAKE

fB insta twitter

U-Heard: Alichojibu Madee kuhusu comment ya Zari kwenye picha yake

U-heard leo May 23, 2017 Soudy Brown ametusogezea moja ya story ambayo imekuwa gumzo mitandaoni kuhusu Zari ambaye ni mpenzi wa staa wa Bongofleva Diamond kuweka comment iliyoibua hisia tofauti kwenye picha ya Madee akiwa Studio za Wasafi.
Soudy amezungumza na Madee ili kujua zaidi kuhusu picha hiyo kuwa na comment nyingi lakini comment ya Zari imeonekana kuwa gumzo zaidi baada ya kuwaambia wamechafua office yake akiwataka waweke viatu chini kwa kuwa walikuwa wamekanyaga ukutani kama sehemu ya pozi la picha.
 Madee Ally amesema kuwa alichokiandika shemeji yake #Zari ni utani tu wa kawaida sana kwao na ameongeza kuwa sikuhizi watu wanashinda sana mitandaoni kiasi kwamba kitu kidogo tu kikitokea wanakikuza na kuonekana kama ni kitu kikubwa sana japo ameonesha kutopendezeshwa na kitendo cha Soudy Brown kufuatilia kitu kisicho na msingi na kusema kuwa anamrudisha kulekule kwa wavaa kanga.
                                               Post iliyoweka gumzo hii hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.