STAA ALIKIBA AWAACHA NJIA PANDA MASHABIKI WAKE
Mkali
wa sauti na mwenye 'hit song' ya 'Aje', Alikiba amewaacha njia panda
watu wake wa karibu pamoja na mashabiki wa kazi zake baada ya yeye
kuweka picha katika mtandao wake wa Instagram ukiwa na neno 'wananiita
Kipusa'
Muda
mchache kupita mashabiki hao walimiminika katika picha hiyo kwa kutoa
maoni yao binafsi, huku wengine wakijaribu kubashiri kuwa huenda ni
ujio wake mpya wa nyimbo anayotarajiwa kuiachia katika siku za hivi
karibuni.
Miongoni mwa ujumbe zilizokuwa zikitawala chini ya tangazo hilo ni pamoja na;
Rajo Jr: Alikiba
bana, katisha na atapita hivi hivi na kutuacha na mihamu yetu hahaha.
King ni 'undefined musician' unaweza kuta kipusa siyo nyimbo ila kauliza
tu kuwa wanamuita kipusa?, kwa sababu tuna hamu ya kumsikia tumewaza
ngoma mpya.
Careen Candy: Nafuu
leo imekua siku nzuri maana ulishaanza kuniboa hata wanangu wakikuona
kwenye runinga walikuwa wakiniita lakini sikuweza kutoka ndani.
Official george :siye tunataka ngoma, hatutaki maneno maana tumechoka kunyanyasika huku mtaani.
Costz himself: Tunavyoijua
'Team' Fulani muda huu watakuwa wanapanga kuishambulia kipusa, na
wahakikishieni Kipusa ikitoka basi na wao wote wataachia ngonjela zao
zinazopigwaga shuleni akija mgeni.
Inno_Kalinga: Waachie washindane na jina la nyimbo kwa wiki mbili kwanza.
Karim Issa: Mungu akusimamie unstoppable utuletee ngoma Kali, maana tumechoshwa na mavuvuzela.
Babesh Sultan: sawa si kwa kutususa hivi king, wengine washapata matatizo ya moyo kusubili ngoma. Iachie mzee baba kitaani hatuna raha kabisa.
Kwa
upande mwingine, hayo yote yametokana na ukimya wa kipindi kirefu cha
Alikiba jambo ambalo limepelekea mashabiki zake kuanza kufurahia jambo
ambalo hata hawalifahamu kiundani kwamba Kipusa ni ujio wa nyimbo yake
mpya au pengine msanii huyo ameamua kubadilisha jina na kujiita hivyo
au pengine ameamua kuja na 'product' zake ambazo zitakuwa zikiitwa kwa
jina hilo.
Alikiba
siku ya Jumamosi anatarajia kufanya show katika mji wa New York,
Marekani ambapo atakuwa na wasanii wengine kama P Square, 2 Face
Idibia, Tiwa Savage pamoja na Cassper Nyovest
No comments:
Post a Comment