Header Ads

Yanga imewatoa Mabingwa wa Kenya SportPesa Super Cup

MuroTV

Yanga imewatoa Mabingwa wa Kenya SportPesa Super Cup

June 5 2017 Mabingwa Ligi Kuu soka Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans walicheza dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Kenya Tusker FC katika mchezo wa SportPesa Super Cup, Yanga wamefanikiwa kuitoa Tusker FC katika michuano hiyo.
Yanga wamefanikiwa kuifunga Tusker FC kwa  mikwaju ya penati 4-2, hivyo ushindi huo umeipeleka Yanga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya SportPesa Super Cup 2017, Yanga sasa watacheza dhidi ya AFC Leopard katika mchezo wa nusu fainali.
Dar es Salaam Young Africans watacheza na AFC Leopard ya Kenya katika mchezo wa nusu fainali, Leopards wao wamefuzu kucheza hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Singida United kwa mikwaju ya penati 5-4, hiyo ni baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati 
 Image may contain: text

KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 

Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
          : prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

No comments:

Powered by Blogger.