UTAFITI: Wanaume waliochelewa kupata watoto, hupata watoto wenye akili
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Seaver Autism Center
ya Marekani umeonesha kuwa Wanaume waliochelewa kupata watoto huwa na
uwezo wa kuzaa watoto wapole, wenye akili na uwezo wa kung’amua mambo
kwa haraka kuliko waliowahi kupata watoto wakiwa katika umri wa kati.
Katika utafiti uliohusisha zaidi ya watoto 7,781 ambao zaidi ya 57%
kati yao walizaliwa na baba wenye umri wa miaka 50 na kuendelea
wameoneka kuwa na akili kubwa za darasani kuliko watoto waliozaliwa na
baba wenye umri wa miaka 25.
Akiliezea namna inavyotokea Dr. Dolores Malaspina alisema wanaume wenye umri mkubwa hupitia kitendo kinachoitwa ‘sperm mutations’ ambapo
mbegu za kiume za mwanaume mzee hubadilika hivyo mimba zinapotungwa
baada ya kitendo hiki kutokea huchangia kuzaliwa kwa watoto wenye akili.
No comments:
Post a Comment