Header Ads

Ronaldo kataja sababu za kubadili style ya nywele zake

Michezo

MuroTV

MICHEZO

Ronaldo kataja sababu za kubadili style ya nywele zake

Kama wewe ni moja kati ya mashabiki wa soka hususani mashabiki wa soka la Ulaya na wanaompenda staa wa soka wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo najua utakuwa ni mmoja kati ya watu waliyomuona na muonekano tofauti kichwani.
Ronaldo ambaye amezoeleka kuwa na tabia ya kupenda kuzitunza nywele zake kiasi cha kufikia kusemwa katika mitandao ya kijamii kuwa anapenda kuziangalia nywele zake sana katika kioo akiwa anaingia uwanjani, alionekana kanyoa siku moja baada ya ushindi wa Champions League.

Leo June 6 2017 mtandao wa bleacher report umemnukuu staa huyo akitaja sababu za kunyoa nywele hizo baada ya ushindi wa 4-1 akiwa kafunga magoli mawili na kuisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa taji la 12 la UEFA Champions League msimu wa 2016/2017.

“Niliweka ahadi mwenyewe kama tutashinda Champions League na nitafunga goli basi nitanyoa nywele zangu tumeshinda na nimefunga”>>> Ronaldo
MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati 
Image may contain: text

KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 

Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
          : prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

No comments:

Powered by Blogger.